Jumatano, 18 Mei 2016

Ni kemikali gani hutumiwa na wahalifu kuvunja vioo vya gari?

Na Syriacus Buguzi

Hivi karibuni nilishuhudia gari la  mama mmoja likiwa limevunjwa kioo kidogo na wahalifu kufanikiwa kuondoka na mkoba wake. Hii ilitokea katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Katika kukitazama kwa ukaribu, nilibaini kwamba kioo kile hakikupigwa kwa nyundo wala jiwe, bali tu kilionekana kama kimeyeyushwa tu.

 
Kioo cha gari kikiwa kimeyeyushwa na wahalifu:PICHA| |MTANDAO


Mpaka sasa sijafahamu ni kemikali ya aina gani ilitumika na hawa wahalifu wanaipata wapi. Swali jingine, je, labda serikali ina mpango gani katika kuithibiti kemikali hiyo?
 

Lakini pia, wale wahalifu  wanatumia kitu gani kubaini kuwa kwenye gani kuna kitu cha thamani kama laptop, simu, tablet nk?

Ili kupata majibu ya maswali haya na mengineyo, tafadhali endelea kutembelea ukurasa huu. Tunakuandalia taarifa za undani zaidi katika swala hili linalo husu usalama wako kama mmiliki wa gari na usalama wa mali zako.